Makundi ya waangalizi wa uchaguzi pamoja na mashirika mengine nchini Kenya yana wasiwasi kuhusu mbinu zilizowekwa kudhibiti mizozo baada ya uchaguzi mkuu ikizingatiwa ushindani mkubwa uliopo. Wadau hao wanapendekeza kuwepo mikakati ikiwemo kufunga baa na maeneo ya pombe ili kudhibiti uwezekano wa ghasia. Sikiliza ripoti ya Wakio Mbogho kutoka kaunti ya Nakuru.