Waasi na jeshi wakabiliana Congo, M23 iko tayari kuondoka
7 Desemba 2022Matangazo
Askari wa Congo walilikabili kundi hilo nje ya mji wa Bwiza, karibu kilomita 40 kaskazini mwa mji mkuu wa mkoa Goma. Duru zinasema makabiliano hayo yalisababisha wakaazi kukimbia na shughuli katika mji jirani wa Kitchanga kusitishwa.
Machafuko hayo ya karibuni katika nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita yanajiri wiki moja baada ya shambulizi lililodaiwa kufanywa na M23 mashariki mwa mkoa wa Kivu Kaskazini kuwauwa karibu watu 300, karibu wote wakiwa ni raia.
Waasi hao wametoa taarifa wakisema wako tayari kujiondoa, ikiwa ni sharti muhimu lililowekwa na Angola kwenye mazungumzo ya amani mwezi uliopita pamoja na nchi jirani Rwanda.