1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi nchini Kongo waua watu 21 wiki ya Krismasi

29 Desemba 2024

Watu 21 waliuawa katika eneo linalozongwa na machafuko la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika wiki ya sikukuu ya Krismasi.

https://p.dw.com/p/4oelY
Kongo | Wanajeshi | Beni | DRC
Vikosi vya usalama vikifanya operesheni ya pamoja ya kijeshi ya Uganda na DRC dhidi ya waasi katika eneo la Beni, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Ni kulingana na vyanzo vilivyoliambia shirika la habari la AFP jana Jumamosi, vikisema mashambulizi hayo yalifanywa na waasi wa ADF, wenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Mashambulizi hayo yalifanywa karibu na mji mdogo wa Manguredjipa unaofahamika kwa utajiri wake mkubwa madini.

Soma pia:  Watu 10 wauawa katika shambulio la ADF mashariki mwa Kongo

Waasi wa ADF ambao mwanzoni walitokea Uganda, wamekuwa wakifanya mashambulizi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu katikati ya miaka ya 90.

Tangu wakati huo, wanamgambo hao wamewaua maelfu ya raia eneo hilo.