Waasi wa M23 wajiimarisha Mashariki mwa Kongo
9 Aprili 2024Taarifa zinasema kuwa wapiganaji hao wa kundi la M23 wamejiimarisha kwenye mlima wa kihuli na kimoka kilometa karibia 5 na mji wa sake ,ambako kikosi hicho cha walinda amani wa umoja wa mataifa kimejiondosha . akiwa na hofu baada ya hatua hiyo ya Monusco ,Pascal Kulimushi anayeishi sasa kwenye kijiji cha mubambiro mbali kidogo na eneo la mapigano aeleza zaidi .
"Hii Monusco kuondoka eneo la kihuli na kimoka ni ishara kwamba kuna njama yakuzipana miji ya Goma na sake mikonani mwa waasi,sababu operesheni ya springbok ilikuwa ikilenga kulinda miji hiyo lakini sasa ni M23 ndio wamechukuwa udhibiti.Tunashangazwa saana na hilo," alisema bwana Kulimushi.
Mapema mwanzoni mwa mwezi wa novemba mwaka uliuopita ,Monusco walitangaza operesheni ya pamoja na jeshi la serikali ya kongo ,iliyolenga kuwazuiya waasi hao wa M23 kuzikamata miji ya Goma na Sake ,operesheni ambayo sasa yaelekea kugonga mwamba. Yedo Matachoka ni mchambuzi wa maswala zakisiasa nchini kongo.
Wanajeshi wanne wa Tanzania wauwawa Kongo
Ujumbe huo wa umoja wa mataifa nchini kongo, ulitolea tahadhari juu ongezeko la idadi ya waasi wa M23 Kwenye mzunguko wa mji wa Sake kilometa 20 kutoka mji mkuu wa jimbo hili ,Goma na kuwa hali hiyo inaweza kuuweka mji huo hatarini. katika siku za hivi karibuni makambi ya wakimbizi nje kidogo na mji wa Goma yamekuwa pia yakilengwa na makombora toka ngome za M23 nakusababisha vifo kwa watu hao wanao hangaika.
Wakati huhuo, kikosi cha jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kimetangaza kuuwawa kwa askari wake wanne kutoka tanzania waliouawa wiki iliyopita baada ya kombora kuiangukia kambi yao eneo la mubambiro.
Tangu mwezi wa Desemba mwaka jana,SADC imewaleta mkoani kivu kaskazini wanajeshi kutoka Afrika kusini,Tanzania na malawi kuiunga mkono serikali ya kinshasa kupambana na wapiganaji wa M23 ,ambao kwa msaada wa jeshi la Rwanda wamefaulu kudhibiti sehemu kubwa za mkoa huu unao shuhudia machafuko mabaya zaidi kuwahi kutukia.
Benjamin Kasembe