Wabunge Korea Kusini wamtimua rais wa pili katika wiki mbili
28 Desemba 2024Rais wa mpito wa Korea Kusini, Han Duck-soo, ameondolewa madarakani na wabunge jana, wiki mbili tu baada ya Rais Yoon Suk Yeol kusimamishwa kutokana hatua yake ya kutangaza sheria ya kijeshi.
Han alikabiliwa na madai ya uchochezi na kukataa kuteua majaji wa ziada katika Mahakama ya Katiba, jambo lililozidisha mgawanyiko wa kisiasa.
Soma pia: Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini kuamua hatma ya Rais Yoel
Waziri wa Fedha Choi Sang-mok amechukua nafasi ya rais wa muda, akiahidi kuleta utulivu, wakati ambapo sarafu ya nchi hiyo, won, ikiporomoka kwa kiwango cha chini zaidi katika miaka 16 na thamani ya hisa kwenye soko la hisa la nchi hiyo, KOSPI ikiporomoka kwa asilimia 1.02.
Upinzani ulidai hatua za Han zilikiuka katiba na kuvuruga mchakato wa kisheria.