Wabunge Thuringia wamchagua spika kutoka CDU
29 Septemba 2024Koenig alikuwa anashindana na mteule wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, Wiebke Muhsal. Alipata wingi wa kura 54 kati ya jumla ya kura 88 kwa kuungwa mkono na vyama vya mrengo wa kati na vile vya mrengo mkali ya kushoto.
Hayo yametokea licha ya chama cha AfD kuibuka cha kwanza katika uchaguzi wa Septemba 1 jimboni Thuringia, kwa kupata asilimia karibu 33 ya kura. Chama cha CDU kilishika nafasi ya pili kwa kupata karibu asilimia 24 ya kura.
Soma pia:Kiongozi wa chama cha CDU Friedrich Merz kugombea ukansela
CDU kinajaribu kuunda serikali jimboni Thuringia kwa kuiweka kando AfD. Ili kuunda serikali ya muungano jimboni humo, CDU inafanya majadiliano na chama cha mrengo wa kati-kushoto cha SPD, na kile kipya cha mrengo mkali wa kushoto cha Muungano wa Sahra Wagenknecht, BSW.