1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini kupiga kura ya kumfungulia mashtaka rais

5 Desemba 2024

Wabunge wa upinzani nchini Korea Kusini wamesema watapiga kura ya kumfungulia mashtaka Rais Rais Yoon Suk Yeol kwa jaribio lake la kutangaza sheria ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4nluP
Seoul | Maandamano | Korea Kusini
Raia wa Korea Kusini wakishikilia mabango yenye maandishi "Tunataka Yoon Suk Yeol afukuzwe" wakati wa maandamano mjini Seoul, Korea Kusini.Picha: Lee Jin-man/AP Photo/picture alliance

Hayo yanajiri wakati waziri wa ulinzi anayeshtumiwa kwa kumshauri rais huyo juu ya kutangaza sheria ya kijeshi akijiuzulu.

Wabunge hao kutoka chama cha upinzani cha Democratic wamepanga kupiga kura bungeni ya kumfungulia mashtaka Yoon siku ya Jumamosi. Haya ni kulingana na msemaji wa chama hicho aliyewaarifu waandishi wa habari.

Awali, mbunge wa chama hicho cha Democratic, Kim Seung-won, aliliambia bunge kwamba tangazo la serikali ya Yoon ya sheria ya dharura ya kijeshi lilisababisha kuchanganyikiwa na hofu kubwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo.

Soma pia: Chama tawala Korea Kaskazini chagawika kuhusu rais 

Chama tawala cha Yoon cha People Power Party kimegawanyika kuhusu mgogoro huo, lakini kimesema kitaipinga kura hiyo.

Chama cha Democratic kinahitaji angalau wabunge wanane kati ya 108 wa chama tawala kuunga mkono hoja hiyo ili ipitishwe na theluthi mbili ya wingi wa kura za bunge hilo lenye viti 300.