Duru nchini Kenya zinasema polisi inawahoji wabunge wawili kuhusiana na machafuko yanayojitokeza huko kaunti ya Laikipia ambako makundi yenye silaha yanaendesha hujuma dhidi ya raia na kupambana na maafisa wa usalama. Rashid Chilumba amezungumza na kamishna wa jimbo la Bonde la Ufa anayesimamia pia kaunti ya Laikipia George Natembeya na kwanza alitaka kujua wamefikia wapi kwenye mahojiano hayo.