Kumekuwa na wimbi la wachezaji mahiri Ulaya kuhamia Uarabuni kwa mvuto wa mishahara mikubwa wanayoahidiwa. Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji wa kwanza wa hadhi ya juu aliyefungua mlango wa wachezaji mahiri wa Ulaya kuelekea huko na klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia iliwasilisha ombi la kumtaka nyota wa PSG Kylian Mbappe. Ili kulijadili hili, Jacob Safari anazungumza na mchambuzi Sekione Kitojo.