1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiJamhuri ya Kongo

Wafanyabiashara wa nishati ya mafuta wagoma Kongo

23 Oktoba 2023

Wamiliki vituo vya kuuza mafuta ya gari Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika majimbo matano ya mashariki waendesha mgomo kushinikiza serikali kupunguza bei, mamlaka yasema bei imepanda kuanzia soko la dunia.

https://p.dw.com/p/4Xujp
Gari kwenye kituo cha mafuta bila muhudumu
Gari kwenye kituo cha mafuta bila muhudumuPicha: Subrata Goswami/DW

Wamiliki wa vituo vya mafuta wanasema wamegoma kwa vile wanahisi serikali haijachukua hatua muhimu katika madai yao ya kutangaza muundo mpya wa bei ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta kwenye ngazi za kimataifa.

Mnamo Septemba 30, wawakilishi wa wamiliki wa vituo vya mafuta walikutana katika mazungumzo na wajumbe wa serikaliya Kongo mjini Lubumbashi ila wenye vituo vya mafuta wanasema tangu hapo hakuna kilichotekelezwa.

Ili kujaribu kupata hata nusu ya mafuta, madereva wanaelekea kwa wauzaji wadogo wadogo wanaojulikana kama kadaffi ambao sasa nao wamewapandisha bei kwa zaidi ya maradufu.

Soma pia:Uhaba wa Mafuta nchini Tanzania

Hatua hiyo imesababisha huduma ya usafiri wa umma kupanda bei, huku baadhi ya watu wenye magari binafsi wameamuwa kuegesha magari yao nyumbani kwa kukosa mafuta.

Serikali: Tunashughulikia changamoto ya mafuta

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Waziri Patrick Muyaya, amethibisha kwamba wamiliki wa vituo vya mafuta walikutana na Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde mnamo tarehe 19 Oktoba, huku pande zote zikitaja upungufu wa faida, na kwamba bado serikali inashughulikia kadhia hiyot.

Soma pia:Uhaba wa mafuta Uingereza waathiri huduma muhimu kama uuguzi

Muyaya amesema serikali inahakikisha kwamba hatua zote zimechukuliwa ili kuhakikisha hali ya ugavi wa nishati ya petro unarejea katika mfumo wake wa kawaida.

Kupanda kwa bei ya mafuta Kenya

"Naibu Waziri Mkuu anaehusika na Uchumi, amepewa jukumu la kukamilisha majadiliano yanayoendelea na washirika hao wa serikali”. Alisema Muyaya

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini Kongo wanansema kupanda kwa bei ya nishati ya petroli inatokana na mzozo wa kati ya Ukraine na Urusi, na pia vita kati ya Israel na Palestina.

Mgomo huo wa wamiliki wa vituo vya mafuta unafanyika katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Tanganyika, Katanga ya Juu na Lualaba.