1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa kiwanda cha Volkswagen wagoma

29 Oktoba 2024

Wafanyakazi wa viwanda vya chuma na kieletroniki wameanza migomo ya kudai nyongeza za mishahara nchini Ujerumani wakati ambapo pana mipango ya kufungwa kwa viwanda vya kampuni ya magari ya Volkswagen.

https://p.dw.com/p/4mL6L
Ujerumani | Volkswagen
Wafanyakazi wa kiwanda cha Volkswagen wagoma kudai nyongeza za mishahara UjerumaniPicha: Erik Schelzig/AP Photo/picture alliance

Jumuiya kuu ya wafanyakazi ya Ujerumani, IG Metall, ilizindua harakati hizo za kudai malipo zaidi na kupinga mazingira mabaya ya kazini kwa migomo iliyoanza usiku wa kuamkia leo.

Wafanyakazi milioni 3.9 wameajiriwa kwenye viwanda hivyo vya chuma na kieletroniki nchini Ujerumani.

Kampuni ya magari ya Ujerumani ya Volkswagen yapanga kufunga viwanda 3

Pana hali ya sintofahamu miongoni mwa wafanyakazi kwenye kampuni ya magari ya Volkswagen kutokana na mipango juu ya kufungwa kwa baadhi ya mitambo, kukatwa mishahara na kuachishwa kazi kwa idadi kubwa ya watu.