1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa Lufthansa waanza mgomo

7 Februari 2024

Msemaji wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Ujerumani (Verdi) amebainisha kuwa wafanyakazi wa shirika la ndege la nchi hiyo, (Lufthansa) wameanza mgomo wao leo katika viwanja kadhaa vya ndege.

https://p.dw.com/p/4c7YJ
Ujerumani | Verdi-Lufthansa- Munich
Mgomo wa wafanyakazi wa shirika la ndege la Ujerumani (Lufthansa) umesababisha maelfu ya safari kufutwa.Picha: Sven Hoppe/dpa/picture alliance

Lufthansa, ambalo ndilo shirika kubwa zaidi la ndege la Ujerumani, limefuta kati ya asilimia 80 hadi 90 ya safari zake 1,000 za ndege zilizokuwa zimeratibiwa siku ya Jumanne (Februari 7).

Mgomo huo ulitarajiwa kudumu hadi saa 1:00 asubuhi ya Jumatano (Februari 8).

Soma zaidi: Mgomo wakwamisha maelfu ya abiria Ujerumani

Viwanja vya ndege vya Frankfurt na Munich ndivyo vilivyoathirika zaidi na mgomo huo huku zaidi ya abiria 100,000 wakitarajiwa kuahirisha safari zao.

Verdi inataka nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi hao wa Lufthansa na pendekezo lililowasilishwa katika raundi ya pili ya mazungumzo mnamo Januari 23 lilikataliwa.