1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa mwanaharakati wa ufisadi waandamana India

22 Machi 2024

Wafuasi wa mwanaharakati mmoja anayepinga ufisadi nchini India ambaye pia ni mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi zaidi nchini humo Arvind Kejriwal, wameandamana kupinga kukamatwa kwake.

https://p.dw.com/p/4e0Sv
Indien | New Delhi
Wafuasi wa mwanaharakati wa India Arvind KejriwalPicha: AP Photo/picture alliance

Wafuasi wa mwanaharakati mmoja anayepinga ufisadi nchini India ambaye pia ni mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi zaidi nchini humo katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Arvind Kejriwal, wamefanya maandamano leo kupinga kukamatwa kwake, hatua ambayo vyama vya upinzani vinasema ni sehemu ya ukandamizaji unaofanywa na serikali ya waziri mkuu Narendra Modi kabla ya uchaguzi mkuu.

Fuatilia: India: Muungano mpya wa upinzani unaweza kumuondoa Modi 2024?

Kejriwal, mkuu mpya wa jimbo la New Delhi, alikamatwa jana usiku na idara ya kuchunguza na kufuatilia kesi zinazohusiana na utakatishaji fedha na rushwa nchini humo inayothibitiwa na serikali ya Modi.

Idara hiyo inakishtumu chama chake na mawaziri kwa kupokea rushwa ya dola milioni 12 kutoka kwa wanakandarasi wa vileo takriban miaka miwili iliyopita.

Chama cha Kejriwal cha Aam Aadmi kimekanusha madai hayo na kusema ni ya kutungwa. Chama hicho kimesema kuwa Kejriwal ataendelea kuwa mkuu wa jimbo la Delhi huku kikikabiliana na mashtaka hayo mahakamani