Wagiriki waandamana kupinga ndoa za jinsia moja
12 Februari 2024Matangazo
Kwa mujibu wa polisi watu wapatao 4,000 waliitikia wito wa vikundi vya kidini vya madhehebu ya Othodoksi. Walikusanyika katikati mwa uwanja wa Syntagma, wakipeperusha bendera za Ugiriki na mabango yanayopinga uhusiano wa jinsia moja. Kanisa la Orthodox la Ugiriki ambalo lina uhusiano wa karibu na wabunge wengi wa chama kilicho serikalini limesema "linapinga kabisa" mageuzi hayo, likisema kwamba "linalaani" watoto kukua katika "mazingira ya tata". Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis, ambaye binafsi anatetea mswada huo, amesisitiza kuwa mabadiliko hayo yatanufaisha "watoto na wanandoa wachache."