1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea 24 wametangaza rasmi kuwa watagombea urais Kongo

9 Oktoba 2023

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, CENI, imesema kuwa wagombea 24 akiwemo Rais Felix Tshisekedi, wametangaza rasmi kuwa watagombea urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba

https://p.dw.com/p/4XH4Q
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi akihudhuria mkutano wa ushirikiano kati ya Uturuki na mataifa ya bara Afrika mjini Istanbul Uturuki mnamo Desemba 18, 2021
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo Felix TshisekediPicha: Isa Terli /AA/picture alliance

Wapinzani wa zamani, wagombea wa mara ya kwanza na wagombea walioshindwa katika chaguzi zilizopita, ni miongoni mwa wale wanaompinga Rais Tshisekedi na kusababisha idadi kubwa ya wagombea ambao wachambuzi wanaamini huenda wakagawanya kura za upinzani na kuimarisha nafasi ya ushindi kwa Tshisekedi.

Soma pia:Ofisi za usajili wa wagombea wa uchaguzi Kongo zafunguliwa

Tume hiyo ya uchaguzi, ilichapisha wasifu wa wagombea hao 24 katika mtandao wa kijamii wa X ambao awali ulijulikana kama Twitter. Mahakama ya kikatiba itathibitisha rasmi orodha ya mwisho katika wiki zijazo.

Mazungumzo yadaiwa kuendelea kumuunga mkono mgombea mmoja wa upinzani

Wakati huohuo, Tresor Kibangula, mchambuzi wa kisiasa katika kituo cha utafiti cha Ebuteliu, amesema mazungumzo yanaendelea miongoni mwa baadhi ya wagombea kuhusu kuungana na kumuunga mkono mpinzani mmoja maarufu.