Wagombea wa uenyekiti wa tume ya AU wataka kiti baraza la UN
14 Desemba 2024Matangazo
Na wakitaka pia uwepo wa maingilia ya kibiashara barani Afrika pamoja na masuala mengine.Katika mdahalo huo wa jana usiku Ijumaa, wa mjini Addis Ababa Ethiopia, RailaOdingawa Kenya, Mahamoud Ali Youssouf wa Djibouti na Richard Randriamandrato wa Madagascar wanatafuta kuchaguliwa katika nafasi ya Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika wenye wanachama 55. Walishiriki wote katika mjadala wa saa mbili walitetea viti viwili vya kudumu kwa Afrika ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuwakilisha mataifa yao.Watatu hao wanajaribu kushawishi nchi nyingi za Kiafrika kabla ya Uchaguzi wa Februari wa kumrithi Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki, ambaye amehudumu kwa vipindi viwili.