JamiiItaly
Ajali ya boti Italia: Wahamiaji 2 wafariki na 20 watoweka
11 Aprili 2023Matangazo
Shirika la misaada la Ujerumani ResQship limesema kwamba, imewaokoa manusura wengine 22 na kuwapeleka katika kisiwa cha Lampedusa, Italia.
Miongoni mwa waliokolewa ni pamoja na wanawake na watoto kutoka katika mataifa ya Cameroon, Ivory Coast na Mali ambao boti yao iling'oa nanga katika bandari ya Sfax Tunisia ikikadiriwa kuwa na abiria zaidi ya 40.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Italia zaidi ya wahamiaji 14,000 wamewasili nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka, kiwango hicho kikitajwa kuwa ni cha juu zaidi ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo wahamiaji 5,300 waliingia nchini humo wakitokea katika mataifa yanayoendelea, wakiingia Ulaya kusaka maisha bora.