1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko unaodaiwa kuwa wa gesi wajeruhi wahamiaji 31 Italia

11 Novemba 2023

Watu 31 wamejeruhiwa baada ya kutokea mlipuko unaodhaniwa kusababishwa na gesi ulioharibu sehemu ya jengo linalotumiwa kama makaazi ya waomba hifadhi kwenye mji wa San Lorenzo Nuovo nchini Italia.

https://p.dw.com/p/4YhNd
Italien | Migranten auf Lampedusa
Wahamiaji wakiwa ItaliaPicha: Cecilia Fabiano/AP Photo/picture alliance

Idara ya zimamoto imesema, mlipuko huo ulitokea muda mfupi kabla ya usiku wa manane, kuamkia leo Jumamosi. Mtu mmoja kati ya waliojeruhiwa alikuwa mahututi na alisafirishwa kwa helikopta kuelekea hospitali mjini Roma kwa ajili ya matibabu.

Idara ya zimamoto ya mji wa San Lorenzo imesema kuna uwezekano mkubwa mlipuko huo umesababishwa na kuvuja kwa gesi na tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini cha halisi cha mkasa huo.

Wengi wa waomba hifadhi wanaoishi kwenye jengo lililoathiriwa na mlipuko huo wengi wao ni wanaume lakini pia wapo wanawake.