1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji wengi waliangamia baharini wakienda Uhispania 2024

26 Desemba 2024

Takribani wahamiaji 10,457 walikufa au kutoweka wakati wakijaribu kuingia Uhispania kupitia baharini katika mwaka wa 2024. Hiyo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50 kutoka idadi ya mwaka wa 2023.

https://p.dw.com/p/4oaws
Wahamiaji wakijaribu kuingia Uingereza
Barabara ya Atlantic ndio inayozingatiwa kuwa hatari zaidi huku maelfu ya watu wakifa kila mwakaPicha: Johan Ben Azzouz/VOIX DU NORD/MAXPPP/dpa/picture alliance

Takribani wahamiaji 10,457 walikufa au kutoweka wakati wakijaribu kuingia Uhispania kupitia baharini katika mwaka wa 2024. Hiyo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50 kutoka idadi ya mwaka jana na idadi kubwa zaidi tangu takwimu hizo zianze kukusanywa.

Soma pia:Miili ya watu 9 yapatikana Tunisia baada ya boti kuzama

Shirika la haki za wahamiaji la Caminando Fronteras limesema katika ripoti kuwa ongezeko hilo la asilimia 58 linajumuisha watoto 1, 538 na wanawake 421. Idadi hiyo inaangalia kipindi cha kuanzia Januari mosi hadi Desemba 5, 2024. Idadi hiyo ni sawa na wastani wa vifo 30 kwa siku, kutoka karibu vifo 18 katika mwaka wa 2023.

Shirika hilo limesema boti mbovu na njia za hatari pamoja na uhaba wa raslimali vinachangia kuongezeka kwa idadi ya vifo vya wahamiaji. Waathirika ni kutoka mataifa 28, wengi wakitokea Afrika, lakini pia kutoka Iraq na Pakistan.