1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakaazi Florida washughulikia uharibifu wa kimbunga Milton

11 Oktoba 2024

Wakaazi wa Florida wameendelea kushughulikia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Milton huku wakitafakari cha kufanya baada ya kimbunga hicho kupiga eneo zima hilo na kuharibu majumba, na kusababisha mafuriko makubwa.

https://p.dw.com/p/4lfZx
USA Fort Pierce | Hurrikan Milton sorgt für Verwüstung
Picha: GIORGIO VIERA/AFP/Getty Images

Kimbunga hicho kiliandamana na upepo mkali. Takriban watu wanane wameuwawa kufuatia kimbunga hicho ambacho watu wengi wamesema wameshukuru kwamba hakikuwa na nguvu kubwa.

Eneo lenye idadi kubwa ya watu la Tampa limenusurika kupigwa moja kwa moja na kimbunga hicho ambacho kilikhofiwa huenda kingekuwa na madhara makubwa sana.

Hata hivyo, uharibifu mkubwa umeshuhudia kwenye maeneo mengi ya jimbo hilo la Florida ambako paa la uwanja wa mchezo wa Baseball liling'olewa huku mifumo ya umeme ikiharibiwa na kuwaacha kizani zaidi ya watu milioni 3.

Ikulu ya Marekani imeahidi kutoa msaada wa serikali.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW