Idara ya polisi nchini Kenya imelikashifu kundi la maafisa wa kitengo maalum cha polisi GSU waliofuzu jana waliojinakili kwenye ukanda wa video wakitoa matamshi ya kudhalilisha. Walisikika wakijigamba na kujitambulisha kama kundi kali zaidi linalofuzu, na sasa wanaingia kukabiliana na umma vilivyo. Sikiliza ripoti ya Wakio Mbogho kutoka Nakuru.