Wakili wa Durov akanusha mteja wake kuhusika na uhalifu
29 Agosti 2024Matangazo
Kituo cha redio cha Franceinfo na televisheni ya BFM vimeripoti leo kuwa Telegram inafuata na kutii kikamilifu sheria za Ulaya kuhusu masuala ya kidijitali.
Kaminski amewaambia waandishi habari kuwa Telegram inasimamia sheria ambazo ni sawa na mitandao mingine ya kijamii.
Hapo jana, jaji wa Ufaransa alitaka Durov achunguzwe rasmi kwa uhalifu uliopangwa kwenye mtandao huo, lakini alimpa mwanzilishi huyo wa Telegram dhamana kwa sharti la kulipa euro milioni 5, kuripoti polisi mara mbili kwa wiki na kutoondoka Ufaransa.
Mwendesha mashtaka wa Paris, Laure Beccuau amesema katika taarifa yake kwamba jaji aligundua palikuwa na sababu za kumchunguza rasmi Durov kutokana na mashtaka ambayo yalisababisha akamatwe siku nne zilizopita.