Wakimbizi kutoka Burundi na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliko katika kambi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma nchini Tanzania wametaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati ili kumaliza machafuko yanayoendelea nchini mwao na hatimaye waweze kurejea makwao. Mwandishi wetu wa Dar es Salaam, George Njogopa aliwatembelea wakimbizi hao na kutuandalia taarifa ifuatayo.