SiasaPakistan
Wakuu wa siasa, jeshi wajadili kitisho cha ugaidi Pakistan
3 Februari 2023Matangazo
Mkutano huo umejiri siku chache tangu mlipuko uliotokea msikini na kuuwa watu zaidi ya 100.
Mtu anaeshukiwa kuwa mfuasi wa itikadi kali alijitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu wakati wa sala ya adhuhuri, katika ngome ya makaazi ya polisi na ofisi za kuzuia ugaidi siku ya Jumatatu.
Waziri Mkuu Shehbaz Sharif akifungua mkutano wa viongozi hao amesema, taifa zima linahitaji kujua jinsi ya kukabiliana na tishio la ugaidi na hatua ambazo zitachukuliwa ili kuondoa wimbi hilo jipya la ugaidi.
Pakistaan imelilaumu kundi la Tahreek-e-Taliban Pakistan, TTP, lilijitenga na kundi la Taliban la Pakistan, kuhusika na shambulio la Jumatatu.