1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakuu wa ulinzi wa ASEAN wataka mapigano Gaza yakomeshwe

15 Novemba 2023

Mawaziri wa Ulinzi wa nchi za Kusini mashariki mwa Asia wametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4Yp7S
Indonesien | ASEAN Flagge in Yogyakarta
Picha: FREEDY TUNGGA/INA Photo Agency/IMAGO

Aidha wameuhimiza ulimwengu kushirikiana katika kutengenezwa maeneo salama ya kupitishwa misaada ya kiutu huko Gaza.

Hata hivyo wakuu hao wa ulinzi wa jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia - ASEAN wameshindwa jinsi ya kuyashughulikia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Myanmar.

Jumuiya ya ASEAN yahofia mizozo mipya

Mzozo wa Myanmar ulikuwa mada kuu wakati mawaziri hao walikutana katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta. Jumuiya hiyo inaijumuisha Myanmar, lakini waziri wake wa ulinzi kwa mara nyingine alizuiwa kushiriki mikutano ya wiki hii kutokana na kushindwa kwa serikali ya kijeshi kutekeleza mpango wa dharura wa vifungu tano uliotayarishwa kwa ajili ya kutuliza machafuko.

Waziri wa Ulinzi wa Indonesia Prabowo Subianto amesema nchi yake imehuzunishwa na kinachoendelea Gaza na inataka mauaji ya raia yakomeshwe.

Jumuiya ya ASEAN haijatoa tamko rasmi kuhusu vita vya Israel na Hamas, ikizingatiwa kuwa kila mwanachama ana msimamo wake kuhusu mgogoro huo.