Serikali ya Kenya imezindua Sera mpya ya Mtaala wa Kitaifa wa Elimu lakini Chama cha Walimu (KUNT) kimeugomea mtaala huo wakidai haukuushirikisha umma kwenye kutayarishwa kwake kama yalivyo matakwa ya kikatiba. Je, walimu wataususia pia mtaala huo kwenye kufundishia wanafunzi? DW imezungumza na Amos Kaburu wa shirika linalojishughulisha na masuala ya elimu Afrika Mashariki, TWAWEZA.