Muungano wa waalimu Kenya, KUPPET, unaitaka serikali iwape walimu wanaosomesha maeneo tete, mafunzo ya kujilinda na kuwapatia bunduki ili waweze kujihami. Ombi hilo linatolewa wakati oparesheni ya usalama ikiwa imeimarishwa huko Kapedo pamoja na baadhi ya wanasiasa wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu wakijisalimisha kutoa taarifa.