Walinzi wa mpaka wa Poland waomba nyogeza ya askari 1,000
7 Agosti 2023Matangazo
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Poland ambaye amesema Mkuu wa Walinzi wa Mipaka ya nchi hiyo, Tomasz Praga, ndiye aliyetuma maombi kwa Wizara ya Ulinzi ya kupatiwa haraka idadi hiyo ya askari wa ziada.
Soma zaidi: Poland imetangaza kuwapeleka wanajeshi mpakani na Belarus
Afisa huyo amesema katika mwaka huu pekee watu wasiopungua 19,000 walijaribu kuvuuka mpaka wa Poland na Belarus, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na watu 16,000 waliofanya hivyo mwaka jana.
Katika wiki za karibuni, Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alilituhumu kundi la mamluki wa kirusi la Wagner kwa kutaka kuteteresha usalama kwenye eneo hilo la mpaka baada ya wapiganaji wake kuonekana upande wa Belarus.