1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Walinzi wa Pwani ya Ufilipino washtumu meli za China

11 Februari 2024

Walinzi wa Pwani ya Ufilipino leo wamezishtumu meli za jeshi za China kwa ''mwenendo hatari'' wakati zilipokuwa zinafanya doria ya siku tisa karibu na Pwani ya nchi hiyo ya Kusini-Mashariki mwa Asia

https://p.dw.com/p/4cGup
Meli ya Walinzi wa Pwani ya China ikisafiri karibu na meli ya Ufilipino (C) ambayo ilikuwa sehemu ya msafara wa boti za kiraia katika Bahari ya Kusini mwa China mnamo Desemba 10, 2023.
Meli ya walinzi wa Pwani ya China Picha: Ted Aljibe/AFP

Taarifa ya walinzi hao wa Pwani, imesema kuwa wakati wa doria hiyo, meli za walinzi wa Pwani ya China (CCG) zilifanya vitendo hatari ikiwemo kuzuia meli ya Ufilipino ya BRP Teresa Magbanua mara nne, na kupita mbele yake mara mbili.

Walinzi wa Pwani ya Ufilipino waelezea kuona ''meli za wanamgambo wa China''

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa meli yake pia "ilizingirwa" na meli nne za walinzi wa Pwani ya China "kwa zaidi ya mara 40".

Walinzi hao wa Pwani ya Ufilipino, pia wanasema waliona kile walichoelezea kuwa "meli nne za wanamgambo wa baharini wa China."

Hata hivyo, ubalozi wa China mjini Manila haukujibu mara moja ombi la tamko kuhusiana na madai hayo.