1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliofariki kwa Kimbunga Chido Msumbiji wafikia 45

18 Desemba 2024

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji imeongezeka na kufikia watu 45.

https://p.dw.com/p/4oJTY
Mosambik | Spuren der Zerstörung, die der Zyklon Chido in Mosambik hinterlassen hat
Picha: UNICEF MOZAMBIQUE/via REUTERS

Idadi hiyo imetolewa na taasisi ya kitaifa ya kudhibiti majanga nchini humo.

Takwimu za awali zilizotolewa jana zimeonyesha kuwa kimbunga hicho kilisababisha vifo vya watu 34 baada ya kuupiga mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado siku ya Jumapili.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, taasisi hiyo ya kitaifa ya kudhibiti majanga imesema watu 38 wamepoteza maisha Cabo Delgado, wanne katika mkoa wa Nampula, na watatu katika eneo la Niassa, sehemu ya ndani kabisa ya taifa hilo. Mtu mmoja bado hajulikana alipo.

Takriban nyumba 24,000 zimeharibiwa kabisa na nyingine 12,300 zimeharibiwa kwa kadri tu huku zaidi ya watu 181,000 wakiathirika na kimbunga hicho.