SiasaAsia
Waliokufa mashambulizi ya msikitini Pakistan wafikia 100
1 Februari 2023Matangazo
Muhammad Ijaz Khan, afisa mkuu wa polisi katika mji huo, amesema hayo mnamo wakati idadi ya vifo imefikia 100 baada ya juhudi za uokozi kumalizika.
Ijaz Khan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kama polisi wako mstari wa mbele dhidi ya wanamgambo, na ndiyo sababu walilengwa.
"Lengo la shambulizi lilikuwa ni kuwavunja moyo." Alisema.
Kati ya maafisa wa polisi 300 hadi 400 walikuwa wakiswali kwenye msikiti huo siku ya Jumatatu wakati shambulizi lilipotokea.
Mashambulizi hudaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo la Taliban la Pakistan na vile vile tawi la kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini humo, lakini shambulizi linalosababisha vifo vingi kama hilo hutokea kwa nadra.