Waliouawa kwa makombora ya Urusi wafikia 11
26 Januari 2024Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Kharkiv imeeleza kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 61 ameuawa leo kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata, na kuongeza idadi ya waliofariki katika mji huo kuwa watu 11.
Katika moja ya mashambulizi makubwa ya angani, zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa na wengine 18 waliuawa baada ya makombora ya Urusi kulenga mji mkuu, Kiev, na mji wa kaskazini mashariki mwa Kharkiv mapema siku ya Jumatatu (Januari 22).
Soma zaidi: Ndege ya kijeshi ya Urusi yaanguka na kuua watu wote 74
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa kujibu kwa nguvu mashambulizi hayo ya Urusi.
Katika tukio tofauti, mamlaka ya Ukraine katika eneo la Donetsk ambayo sehemu yake iko chini ya udhibiti wa Urusi, imesema watu sita wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Urusi jana Alhamisi.