Wamalawi wanapiga kura kumchagua rais
23 Juni 2020Matangazo
Wananchi wa Malawi wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais unaorudiwa baada ya mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka mmoja uliopita. Mahakama ya katiba hapo Februari 3 iliamuru kuwa uchaguzi huo urudiwe, ikiamua kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwanzo yamebatilishwa kwasababu ya ushahidi mkubwa wa mapungufu pamoja na kughushi kura katika uchaguzi uliofanyika Mei 2019.
Mahakama ilibatilisha ushindi wa rais aliyeko madarakani Peter Mutharika ikielezea ushahidi mkubwa wa udanganyifu katika upigaji kura, ikiwa ni pamoja na maelfu ya kura ambazo zilionekana kubadilishwa kwa kutumia wino wa kufanyia masahihisho. Hukumu hiyo ilikubaliwa na mahakama kuu.