Rais mteule Donald Trump ataapishwa kuwa rais wa 47 wa Marekani. Hafla ya kuapishwa imefuatiliwa kote duniani, huku wasiwasi ukihanikiza barani Ulaya kuhusu Uongozi huo mpya wa Marekani. Saumu Mwasimba alizungumza na mchambuzi wa siasa za ndani ya Marekani Mubelwa Bandio, akiwa Maryland na kwanza akamuuliza, Wamarekani wanatazama vipi kuingia huku madarakani kwa Trump?