Wanaharakati wa demokrasia ya Hong Kong kuhukumiwa
30 Mei 2024Majaji watatu wa mahakama kuu wanatarajiwa kuchukua hadi siku mbili kutoa uamuzi huo, huku washtakiwa 47 wakikabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za njama ya kuhujumu mfumo wa serikali.
Soma pia:Sheria mpya ya usalama Hong Kong yaanza kutumika kuanzia leo
Washtakiwa 16 wakiwemo wanaharakati, wabunge wa zamani na madiwani wa wilaya wamepinga mashtaka hayo na hukumu dhidi yao itatolewa wiki hii.
Baadhi ya washtakiwa walikiri makosa
Washtakiwa wengine 31 walikiri makosa wakitarajia adhabu ndogo. Washtakiwa wengi wamezuiliwa gerezani tangu walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Machi 2021.
Soma pia:China yawakemea wanaokosoa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong
Eric Lai, mtafiti katika Kituo cha Sheria za Asia cha Chuo Kikuu cha Georgetown, amesema uamuzi wa leo utaonyesha ikiwa Hong Konginachukulia ushiriki wa kisiasa usio na vurugu kuwa uhalifu.