1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Wanaharakati wamkosoa rais wa Tunisia

22 Februari 2023

Kundi maarufu la kutetea haki za binaadamu nchini Tunisia, linamtuhumu Rais wa nchi hiyo Kais Saied kwa kile wanachokiita "ubaguzi wa rangi na matamshi ya chuki".

https://p.dw.com/p/4Nq4J
Tunesien Tunis | Protest gegen Kais Saied
Picha: FETHI BELAID/AFP

Kundi maarufu la kutetea haki za binaadamu linamtuhumu Rais wa Tunisia Kais Saied kwa kile wanachokiita "ubaguzi wa rangi na matamshi ya chuki".

Kauli hiyo imetolewa baada ya Rais Saied kuapa kuwachukulia hatua kali wahamiaji wa Afrika wanatokea katika mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Saied, ambaye amejinyakulia karibu mamlaka yote tangu Julai 2021 dhidi ya bunge, amelitaka baraza lake la usalama la kitaifa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na wimbi la wahamiaji.

Msemaji wa jukwaa lenye kujihusisha na Haki za Kiuchumi na Kijamii nchini Tunisia, FTDES, Romdhane Ben Amor, amesema Rais Saied anatumia wimbi la wakimbizi kukwepesha zingatio la uchumi na matatizo ya kijamii.

Tunisia, ambayo iko karibu kilomita 150 kutoka kisiwa cha Italia cha Lampedusa, ni sehemu muhimu ya wahamiaji wa Kiafrika wanaotaka kufika Ulaya kwa kile ambacho Umoja wa Mataifa unasema ni yenye kugharimu maisha ya  wahamiaji zaidi duniani.