1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIraq

Wanamgambo 15 wa kundi la IS wauwawa Iraq

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Kulingana na taarifa ya Kamandi kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM, Wanamgambo hao waliuwawa Ijumaa(30.08.2024) magharibi mwa Iraq.

https://p.dw.com/p/4k82U
Wanajeshi wa Marekani na Iraq wamewauwa wanamgambo 15 wa Dola la Kiislamu nchini Iraq kufuatia operesheni ya pamoja
Wanajeshi wa Marekani na Iraq wamewauwa wanamgambo 15 wa Dola la Kiislamu nchini Iraq kufuatia operesheni ya pamojaPicha: Timothy L. Hale/ZUMA Wire/picture alliance

Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia jukwaa la X imeongeza kuwa wanajeshi saba wa Marekani wamejeruhiwa wakati wa operesheni hiyo. Operesheni hiyo ya pamoja  iliwalenga viongozi wa kundi hilo la dola la Kiislamu.

Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani imebainisha kuwa, wakati wa makabiliano, wanamgambo wa kundi hilo walikuwa wamejihami kwa silaha kadhaa yakiwemo mabomu na mikanda inayotumika kujitoa mhanga.

Operesheni hiyo imefanyika ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mazungumzo kati ya Washington na Baghdad, yaliyojadili ushirikiano wa kijeshi katika kupambana na ugaidi nchini Iraq.