Wanamgambo waua takriban watu 23 mashariki mwa DRC
23 Juni 2024Matangazo
Sababu ya mashambulizi hayo haikuwa wazi ingawa vurugu za wanamgambo nchini Kongo zinahusishwa na mashindano ya muda mrefu ya kuwania ushawishi na utajiri wa rasilimali za madini katika eneo hilo.
Kundi lenye kufahamika kama Ushirika wa Maendeleo ya Kongo (CODECO) moja kati ya makundi mengi yenye kujihami kwa silaha ndilo ambalo linatajwa kuhusika kwa mauwaji ya Alhamisi na Ijumaa katika maeneo ya Djugu.
Kwa mujibu wa ripoti ya ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa wa Kongo, iliyotolewa Machi CODECO, kundi la ADF na wanamgambo wengine wanahusika katika matukio mengi ya mauwaji ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.