1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake wasionyonyesha kwa miezi sita wanaongezeka duniani

7 Julai 2022

Wakati hospitali barani Ulaya zikihamasisha unyonyeshaji wa watoto wachanga, akina mama wanaojifungua nchini Kenya hawaoni jitihada hizo, ingawa si wote wana uwezo wa kumudu maziwa mbadala.

https://p.dw.com/p/4DnKy
Baby, Neugeborenes
Picha: Angel Santamaria/Addictive Stock/imago images

Wanawake wengi duniani huanza kunyonyesha baada ya kujifungua, lakini ni asilimia 44 tu ndio hunyonyesha hadi miezi sita baada ya kujifungua, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Watoto wachanga hawawezi kula chakula kigumu katika miezi sita ya mwanzo wa maisha yao, hutegemea maziwa ya mama au maziwa mbadala. Hii imepelekea uhaba wa maziwa mbadala nchini Marekani, ambapo mtoto mmoja  kati ya wanne ndio hunyonyeshwa maziwa ya mama pekee hadi miezi sita.

Uhaba wa maziwa mbadala umesababishwa na masuala ya uzalishaji na usambazaji.Uchunguzi uliofanywa na mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani katika kiwanda kinachozalisha maziwa mbadala ya watoto, Abbott Nutrition, kiwanda hicho ni moja ya  kampuni nne ambazo kwa pamoja huzalisha takriban asilimia 90 ya maziwa mbadala ya watoto kwenye soko la Marekani. Ingawa uzalishaji ulianza kuongezeka, Abbott Nutrition  imelazimika kusitisha uzalishaji kutokana na dhoruba iliyotokea juni 13, kwenye kiwanda hicho huko Michigan.

Umuhimu wa mama kunyonyesha

Utafiti unapendekeza kwamba kunyonyesha maziwa ya mama pekee ni njia yenye afya na asilia kwa wanawake kuwapa chakula watoto wao wachanga. Ni njia nzuri ya kuboresha uhusiano wa mama na mtoto mchanga na ni  gharama ndogo kuliko maziwa mbadala .

Kwa miongo kadhaa, WHO imeshinikiza hospitali kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama pale mtoto anapozaliwa.Saa 24 za  mwanzo ni muhimu kwa mtoto kujifunza jinsi ya kunyonya moja kwa moja kutoka kwa mama yake.

Hospitali nyingi nchini Marekani na Ulaya wanahamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.Ingawa sehemu nyingine duniani, hawahamasihsi mara kwa mara.

Kwanini wanawake wengi hawanyonyeshi?

Antonina Mutoro, mtafiti wa masuala ya uzazi na watoto katika  Kituo cha Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya barani Afrika mjini  Nairobi nchini Kenya, alifanya uchunguzi katika makazi yasiyo rasmi yaliyopo Nairobi, ambapo ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa iliita "makazi duni na yasiyo salama duniani."

 Akina mama waliojifungua walihojiwa, ambapo asilimia mbili tu ndio hunyonyesha watoto bila kutumia chupa.

 Licha ya kwamba wanawake wengi ambao Mutoro alikutana nao hawawezi kumudu gharama za maziwa mbadala, Wamekuwa wakitumia maziwa ya ng'ombe au vyakula kama vile uji kuwalisha watoto wao kabla ya kufikia umri wa miezi sita, alisema.

Mutoro alisema kwamba, kukosekana kwa unyonyeshaji katika makazi hayo kunatokana na  wanawake hao kutokujifunza kunyonyesha wakiwa  hospitalini baada ya kujifungua.

Wakati mwingine, wanawake huambiwa na madaktari kwamba hawana maziwa ya kutosha. Mutoro alisema uwezo wa mwanamke kuzalisha maziwa ya mama hutegemea mahitaji. Muda mfupi baada ya mtoto  kuzaliwa, anawekwa kwenye maziwa ya mama na husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa.

"Lakini wanawake wanaona ni kawaida kusema ', sina maziwa ya kutosha.' na sulihisho ni kutafuta maziwa mbadala kwani ni chaguo la haraka zaidi," Mutoro alisema.

Si kwasababu ya kutokujua, Mutoro aliongezea, wahudumu wengi wa afya kwenye idara ya magonjwa ya watoto na wanawake wanajua umuhimu wa kunyonyesha kwa mtoto. Lakini hakuna uhamasishaji kutokana na wahudumu kulemewa na kazi, baadhi ya madaktari na wauguzi hawana muda wa kuwafundisha akina mama wanaojifungua kama wanauwezo wa kumudu maziwa mbadala.

Maziwa mbadala yamechochea wanawake kutokunyonyesha

Mnamo 1981, Baraza la Afya duniani, chombo kinachofanya maamuzi ya WHO,ilipitisha kanuni ya uuzaji wa kimataifa kwa bidhaa za mbadala wa maziwa ya mama. Kanuni hiyo ilipiga marufuku uuzaji wa maziwa mbadala , kwa lengo la kuzuia wanawake kutokunyonyesha..

Lakini ripoti ya WHO iliyochapishwa mwezi wa Februari inaonyesha kuwa kampuni zimeendelea kutangaza bidhaa kwa njia ya  mtandaoni, kwani njia hiyo haikuwepo wakati wa kupitisha kanuni hiyo.

Ripoti  imesema kwamba wakati viwango vya unyonyeshaji vimeshuka katika miongo minne tangu kutekelezwa kwa kanuni hiyo, mauzo ya maziwa mbadala   yameongezeka maradufu.