1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waokoaji waendelea kupambana kuwafikia manusura wa kimbunga

15 Machi 2023

Waokoaji wameendelea kupambana kuwafikia manusura katika mji ulioharibiwa wa Blantyre nchini Malawi, baada ya kimbunga Freddy kupiga kusini mwa Afrika kwa mara ya pili, na kusababisha mafuriko ambayo yamewauwa watu 250.

https://p.dw.com/p/4OirR
Mosambik | Zerstörung durch Zyklon Freddy
Picha: ALFREDO ZUNIGA/UNICEF /AFP

Hali ya hewa ilitarajiwa kuimarika wakati kimbunga hicho kikihama kutoka nchi kavu baada ya siku kadhaa za mvua kubwa, lakini ngurumo za radi zitaendelea, na viwango vya mafuriko vitasalia juu katika badhi ya maeneo, hali inayoathiri juhudi za uokozi.

Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Malawi Felix Washoni amesema waliwapata watu kwenye miti, kwenye mapaa ya nyumba au katika maeneo ya miinuko.

Soma pia:Waliokufa kwa kimbunga Malawi na Msumbiji wapindukia 200

Karibu watu 190 wamekufa Malawi huku 584 wakijeruhiwa na 37 hawajulikani waliko. Katika nchi jirani Msumbiji, watu 21 wameripotiwa kufa.