1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura milioni 18 wanamchagua rais nchini Ghana

7 Desemba 2024

Zaidi ya wapiga kura milioni 18 waliojiandikisha wanashiriki kupiga kura Jumamosi kwenye uchaguzi mkuu nchini Ghana. Licha ya kinyang'anyiro kikali cha kuwania urais, wachambuzi wanatarajia matokeo ya amani.

https://p.dw.com/p/4ns80
Ghana I Uchaguzi mkuu
Polisi nchini Ghana akipiga kura yake katika uchaguzi mkuu nchini humoPicha: Julius Mortsi/ZUMAPRESS/picture alliance

Zaidi ya wapiga kura milioni 18 waliojiandikisha wanashiriki kupiga kura Jumamosi kwenye uchaguzi mkuu nchini Ghana. Licha ya kinyang'anyiro kikali cha kuwania urais, wachambuzi wanatarajia matokeo ya amani. 

Wagombea 11 wanawania wadhifa wa rais lakini hata hivyo wagombea wakuu ni makamu wa rais Mahamadu Bawumia, kutoka chama tawala cha New Patriotic Party (NPP), na John Dramani Mahama kutoka chama cha National Democratic Congress (NDC).

Soma zaidi. Wananchi wa Ghana wanapiga kura ya kumchagua rais
Mahama anagombea kwa mara ya tatu.  Alijaribu mnamo mwaka 2016 na mwaka 2020 huku Makamu wa Akufo-Addo, Mahamadu Bawumia, akitarajia kuongeza muda wa chama tawala kusalia madarakani katika uchaguzi wa mwaka huu.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi na vitafungwa majira ya saa kumi na moja jioni kwa saa za Ghana. Matokeo ya awali yataanza kutangazwa jioni hii huku matokeo rasmi ya kwanza yakipangwa kutolewa siku ya Jumanne.