1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wapinzani waanzisha mgomo baridi Myanmar

Hawa Bihoga
10 Desemba 2021

Raia wameanzisha mgomo baridi uliosababisha kufungwa kwa biashara na kuiacha mitaa ikiwa mitupu katika jaribio la karibuni la kupinga mapinduzi ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/446GP
Myanmar Stiller Streik Protest Internationaler Tag der Menschenrechte
Picha: AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa vyombo vya habari katika taifa hilo ambalo lipo chini ya utawala wa kijeshi, barabara na mitaa imeachwa mitupu katika miji mingi huku magari machache yakishuhudiwa katika miji mikubwa ikiwemo Yangon.

Kaung Satt ambae ni mkaazi wa mji wa Yangon mwenye umri wa miaka 25 alifunga duka lake na kushiriki kama sehemu ya kushiriki mgomo huo, ameliambia shirika la habari la ujerumani DPA, amefanya hivyoi kuelezea hisia zake namna ambavyo anauchukia utawala wa kijeshi uliochukua hatamu kutoka kwa utawala wa kiraia.

Ripoti za ndani za Myanmar zinaonesha kuwa mgomo huo baridi unaofanywa nchi nzima umekuwa na mafanikio mno.Kiongozi wa mgomo huo Khin Sander amekiambia chombo kimoja cha habari nchini humo kwamba, dhima za maandamano hayo ni kutaka kuuonesha ulimwengu kuwa hali ya kibinaadam katika taifa hilo ni mbaya sana.

Shinikizo dhidi ya uongozi wa jeshi

Mgomo baridi nchini Myanmar leo Ijumaa 10.12.2021
Mgomo baridi nchini Myanmar leo Ijumaa 10.12.2021Picha: REUTERS

Viongozi wanaoratibu hatua hiyo wameendelea kuwatolea mwito watu washiriki kile walichokiita mgomo wa kimya kimya kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni leo ijumaa, lakini takriban kila shughuli mbalimbali  zimefungwa mapema leo.huku  kazi za sanaa nazo katika maeneo mbalimbali zimeonesha kuunga mkono mgomo huo kupitia michoro ilioshuhudiwa.

Mgomo sawa na huo ulifanyika mwezi Machi, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi, ambapo watu wengi walisalia majumbani na kukataa kufanya shughuli zozote. Tangu wakati huo Myanmar ilitumbukia katika vurugu na machafuko, ambapo jeshi limekuwa likifanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya waandamanaji na raia ili kupinga shughuli za wapinga mapinduzi.

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu  la chama cha wafungwa wa kisiasa, linaloorodhesha  mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu watu wasiopungua elfu kumi na tatu wameuwawa na zaidi za watu elfu kumi wamekamatwa tangu kutokea kwa mapinduzi hayo.