1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Karibu wanajeshi 15 wauawa nchini Mali

17 Agosti 2024

Karibu wanajeshi 15 wameuawa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na kundi la kigaidi lenye mahusiano na al-Qaeda katika eneo la Mopti nchini Mali.

https://p.dw.com/p/4jZRP
maktaba I Mali Bamako
Viongozi wa kundi la waasi nchini Mali la Ansar Dine wakiwa kwenye mazungumzo na mpatanishi mkuu Burkina Faso na viongozi wa kundi jingine la waasi la TuaregPicha: Ahmed Ouba/AFP/Getty Images

Maafisa watatu wa eneo kulikotokea shambulizi wameliambia shirika la habari la AFP jana Ijumaa kwamba wanajeshi hao wameuawa katika shambulizi la kushtukiza lililofanywa na kundi linalounga mkono Uislamu na Waislamu.

Mmoja ya maafisa hao ambaye hakutaka kutambulishwa kutokana na sababu za kiusalama, amesema wanajeshi wengine walijeruhiwa na hawajulikani walipo.

Duru za jeshi zimeliambia AFP kwamba baadhi ya washambuliaji pia waliuawa.

Mali imegubikwa na mashambulizi ya jihadi na makundi mengine yenye silaha kwa zaidi ya muongo mmoja, huku mengi ya mashambulizi hayo yakifanywa katikati ya nchi.