1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bodi ya Benki ya Dunia kuamua hatima ya Wolfowitz

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1J

Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia hii leo itaendelea kujadiliana kuhusu hatima ya rais wa benki hiyo,Paul Wolfowitz.Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo kwa waandishi wa habari haikueleza zaidi.Lakini ripoti za hapo awali ziliashiria kuwa bodi hiyo ilikuwa ikijadiliana na wakili wa Wolfowitz,makubaliano kuhusu njia ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo.Siku mbili kabla,ripoti ya jopo maalum ilisema Wolfowitz amekiuka maadili ya benki hiyo.Wolfowitz amelaumiwa vikali na serikali za nchi za Ulaya,hasa kwa kuchukua hatua ya kumpandisha cheo na kumpa nyongeza kubwa ya mshahara mpenzi wake,muda mfupi tu baada ya kiongozi huyo kushika wadhifa wake katika Benki ya Dunia miaka miwili iliyopita.