WASHINGTON-Bush amteua Naibu Waziri wake wa Ulinzi kuwa Mkuu mpya wa Benki ya Dunia.
17 Machi 2005Matangazo
Rais George Bush wa Marekani,amemteua Naibu Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Paul Wolfowitz kuwa mkuu mpya wa Benki ya Dunia.Benki ya Dunia inagharamia miradi mikubwa ya maendeleo katika kila pembe ya dunia na kiongozi wake kwa kawaida huteuliwa na Marekani.Bwana Wolfowitz ni mmoja ya watu walioandaa mipango ya awali ya kuivamia Iraq.
Wachunguzi wa mambo wanaona uteuzi wake katika nafasi hiyo muhimu duniani,huenda ukasababisha mgawanyiko mwengine baina ya Mataifa ya Ulaya na Marekani,kutokana na Marekani kuonekana inatumia zaidi maamuzi ya kibabe kueleka sera zake za nje.