1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush awataka makachero wa CIA kuacha kutumia mateso dhidi ya watuhumiwa.

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgh

Rais wa Marekani George W. Bush ameamuru kuwa mawakala wa shirika la ujasusi la CIA wafuate sheria za mkataba wa Geneva kuhusu mateso.

Miaka mitano baada ya kuwaondoa wanachama wa kundi la kigaidi la al Qaeda na Taliban kutoka katika ulinzi wa mkataba huo wa Geneva , Bush ametia saini amri ya kiutawala inayolitaka shirika hilo la ujasusi kutekeleza makatazo dhidi ya ukatili, dhidi ya ubinadamu ama mambo ya udhalilishaji kama yaliyoainishwa katika mkataba huo kifungu cha tatu.

Bush amekuwa akikumbana na mbinyo nyumbani na nje ya nchi hiyo juu ya mbinu zinazotumika dhidi ya watuhumiwa wapiganaji wanaoshikiliwa na CIA katika jela za siri pamoja na maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na jela ya kijeshi ya Marekani Guantanamo Bay nchini Cuba.