SiasaIraq
Iraq na Marekani zaanza mazungumzo ya kuondoa vikosi Iraq
27 Januari 2024Matangazo
Ofisi ya Waziri Mkuu Mohamed Shia al-Sudani imesema kwenye taarifa kwamba kiongozi huyo amefungua mazungumzo hayo yanayozikutanisha pande zote mbili ili kwa lengo la kuhitimisha operesheni ya vikosi vya muungano wa kimataifa nchini Iraq.
Baghdadinataraji kwamba majadiliano hayo yataibua mpango wa kupunguza uwepo wa vikosi hivyo, na mshauri wa mambo ya nje wa Sudani, Farhad Alaadin amesema urefu wake utatokana na makubaliano na hatua zitakazokuwa zimefikiwa.
Washington ilisema siku ya Alhamisi kwamba imekubaliana na Baghdad juu ya kuanzishwa kwa "vikundi kazi vya wataalamu wa kijeshi na wataalamu wa ulinzi" kama sehemu ya Tume ya Juu ya Kijeshi iliyoundwa kwa ajili ya mazungumzo na Baghdad.