1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:NASA yavumbua maji Mars

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClm

Taasisi ya Marekani ya Uchunguzi wa Anga NASA inatangaza kuwa imepata ushahidi unaonyesha kuwa huenda sayari ya Mars ina maji.Taasisi hiyo imetoa picha zinazoonyesha kuwa kuta za milima miwili kwenye sayari hiyo zinaonekana kana kwamba zimebadilika kwasababu ya mchiririko wa maji hivi karibuni.

Awali wanasayansi walibaini kwamba barafu na mvuke vinapatikana katika sayari ya Mars ila uwepo wa maji ndio unaoweza kuruhusu viumbe kuishi.Katika siku za mbeleni mitaro iligunduliwa katika sayari hiyo japo uvumbuzi wa sasa unaonyesha kuwa maji hayo yamechiririka hivi karibuni.