Wasiwasi juu ya ongezeko la wagonjwa wa mpox barani Afrika
28 Agosti 2024Africa CDC imeeleza kuwa bara hilo limeorodesha wagonjwa wapya 4,000 wa homa ya nyani wiki iliyopita huku ikitoa wito wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo ambazo zilitarajwa kuwasili wiki hii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, japo zimechelewa.
Mkuu wa kituo hicho cha kudhibiti magonjwa barani Afrika daktari Jean Kaseya, amesema watu 81 wamefariki kutokana na ugonjwa huo wiki iliyopita barani Afrika na kufikisha idadi jumla ya vifo 622 na wagonjwa 22,863.
Soma pia: Viongozi wa WHO wanakutana nchini Kongo kujadili Mpox
Umoja wa Ulaya na Marekani zimeahidi kutoa dozi 380,000 za chanjo dhidi ya homa ya nyani kwenda barani Afrika.
Idadi hiyo hata hivyo ni chini ya asilimia 15 ya dozi ambazo mamlaka imesema inahitaji ili kukabiliana na mlipuko wa homa ya nyani nchini Kongo, kitovu cha dharura ya afya ya umma duniani.