Wasiwasi waendelea kuhusu simu hatari ya Galaxy note 7
13 Oktoba 2016Kampuni ya vifaa vya eletroniki ya Samsung imetangaza kuwatumia wateja wake walioko Marekani makasha yanayoweza kustahimili moto, kama tahadhari dhidi ya uwezekano wa kutokea moto au kulipuka kwa simu zake aiana ya Galaxy Note 7 walizorejesha kwa wauzaji simu hizo nchini humo. Makasha hayo hasa yanatolewa kwa wateja walionunua simu hizo katika tovuti yake ya Samsung.com.
Walio na simu hiyo aina ya Galazy Note 7 pia wameshauriwa kutembelea tovuti ya Samsung kufahamu maelekezo ya kuzirejesha. Kampuni hiyo ya Samsung imetangaza kusitisha utengenezaji wa simu hiyo ya Galazy note 7 miezi miwili baada ya kuizindua upya, baada ya kurekebishwa mara ya pili, kufuatia ripoti kadhaa za simu hiyo kushika moto.Samsung sasa italazimika kupokea zaidi ya Galazy Note 7 million 1.5 ilizokuwa tayari imeuza au kutoa kama simu mbadala. Nyingi ya simu hizo ziliuzwa Marekani na Korea Kusini. Hata ipo video youtube ambayo iliwekwa siku ya Jumanne(11.10.2016) inayomwonyesha mwanamume mmoja kutoka ofisi ya XDA developer nchini Marekani, akitoa maelekezo jinsi ya kuhakikisha usalama wa simu kabla ya kusafirishwa tena Korea kusini.
Makampuni yanayotoa huduma za usafiri wa meli yanaripotiwa kutotaka kuzisafirisha simu hizo aiana ya Galazy Note 7 kutokana na wasiwasi wa kutokea moto.Hata hivyo kampuni ya Samsung imesema makasha iliyotuma kutumiwa katika kuzirejesha simu hizo ni ya viwango vilivyowekwa na Marekani vya usafirishaji Betri ya Lithium-ion au vifaa vingine vinavyopaswa kurejeshwa.Sasa kama zilivyo kampuni kama Tylenol, Ford Pintos na nyingine nyingi zilizojipata katika hali kama hiyo baada ya bidhaa zake kutiliwa shaka, Samsung inalazimika kujaribu kurejesha imani kwa kwa wateja inapojitahidi kuondoa wasiwasi kuhusu bidhaa zake. Hisa za kampuni hiyo zimeshuka na kufikia asilimia nane mjini Seoul, hali ambayo hajawahi kushuhudiwa tangu mwaka 2008 kulipotokea mgogoro wa kifedha, baada ya kampuni hiyo kuomba radhi kwa kusimamisha mauzo ya simu hiyo aiana ya Galazy Note 7.
Baadhi ya wateja wanailamu kampuni ya Samsung kwa kutoshughulikia ipasavyo kasoro zilizojitokeza katika simu hiyo ya Galazy 7. Hahm Young-kyu, mwenye umri wa miaka 43 na ambae bado mkewe anaitumia simu hiyo aina ya Galazy note 7 anaeleza kwa masikitiko makubwa kuwa waundaji simu hiyo kwanza walijaribu kuyaficha mapungufu yake baada ya kutolewa malalamiko. Awali simu hiyo ilikuwa imepokea sifa chungu nzima kutokana na ukubwa wake, mambo mengi iliyonayo na ukubwa wa betri. Hivi sasa itajitahidi kufahamu ni nini hasa kilichokwenda kombo.
Watahitajika kuichunguza simu hiyo kwa makini mambo yote ya kisimsingi kuanzia ndani,nje na hata betri alisema Park Chul Wan. Park, mkurugenzi wa zamani wa kituo cha utafiti wa betri nchini Korea kusini. Park amesema matatizo yanayoikumba simu aina ya Galazy note 7 ni zaidi ya kasoro ya betri. Samsung inahitaji kurejesha tena imani yake kwa wateja kufikia wakati itakapozindua simu yake aiana ya Galaxy S8 mwishoni mwa majira ya baridi au mapema mwaka ujao.
Mwandishi:Jane Nyingi/APE/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga